UKRANE IMESEMA URUSI IMERUSHA KOMBORA LA "INTERCONTINENTAL " VITANI


 Urusi imerusha kombora la masafa marefu kwa Mara ya Kwanza Vitani kutoka eneo la kusini mwa Astrakhan katika shambulio la kulipiza kisasi dhidi ya Ukraine tarehe 21 Novemba 2024 siku ya Alhamisi leo asubuhi. Ni mara ya kwanza Moscow imetumia kombora hilo lenye nguvu na la masafa marefu katika vita hivyo.


Hata hivyo, afisa wa Marekani amepinga madai ya Ukraine na kusema kuwa ni kombora la balistiki lakini si kombora la masafa marefu, imeripoti CBS News. Shambulio hilo la anga linakuja baada ya Ukraine kutumia makombora yaliyotengenezwa na Marekani na Uingereza kushambulia maeneo ya kijeshi ndani ya ardhi ya Urusi wiki hii, na hivyo kuzidisha mzozo ambao tayari umedumu kwa siku 1,000. 


Kombora la balestiki la kuvuka mabara, halijawahi kutumika katika mapigano hapo awali, lililenga miundombinu muhimu katika jiji la kati la Ukrain la Dnipro, wamesema maafisa, wakikataa kufichua uharibifu uliosababisha.

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA