DAR ES SALAAM KUANZA BIASHARA SAA 24 KUANZIA JANUARI 2025


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, Disemba 23,2024 ametangaza mpango wa kuruhusu biashara kufanyika masaa 24 jijini Dar es Salaam kuanzia Januari 2025. Mpango huu unalenga kuongeza mzunguko wa uchumi na kuimarisha nafasi ya Dar es Salaam kama kitovu cha biashara nchini na kanda nzima.


Kariakoo linatarajiwa kuwa kitovu cha utekelezaji, kutokana na umuhimu wake kwa wafanyabiashara wa ndani na mataifa jirani. Mwongozo rasmi wa utekelezaji utatolewa hivi karibuni ili kuhakikisha mpango huu unatekelezwa kwa mafanikio.



Akizungumza na waandishi wa habari, Chalamila alisema kuwa serikali inatarajia kutoa mwongozo mzuri wa ufanyaji biashara na utekelezaji wa mpango huo kabla ya kuanza rasmi Januari 2025. 


Aliongeza kuwa Dar es Salaam ina uwezo wa kuendesha biashara saa 24, na kwamba Kariakoo, kama soko linalohudumia mataifa jirani, litachangia kuimarisha uchumi wa mkoa huo. 


Uzinduzi mkubwa wa biashara kufanyika masaa 24 unatarajiwa kufanyika Kariakoo mwezi Januari 2025.


Wadau wa biashara na wananchi wamehimizwa kushirikiana katika kuufanikisha mpango huu wa kihistoria.

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA