MATUMIZI BORA YA NISHATI KUINUA UCHUMI EAC NA SADC

 


Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo, amesema matumizi bora ya nishati ni msingi wa kukuza uchumi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) zinazotegemea biashara na viwanda.


Akifunga Mkutano wa Kikanda wa Matumizi Bora ya Nishati 2024, 05, Dec jijini Arusha, Waziri Jafo ameipongeza Wizara ya Nishati na wadau mbalimbali kwa kuratibu mkutano huo, akisisitiza ushirikiano wa kikanda katika teknolojia na tafiti za matumizi bora ya nishati.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Khatibu Kazungu, amebainisha kuwa mkakati wa matumizi bora ya nishati umeanza kutekelezwa kwa mipango na bajeti za kila mwaka ili kuhakikisha wananchi na viwanda wananufaika. Sekta binafsi pia imeahidiwa kushirikishwa kikamilifu.

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA