RADI YATEKETEZA WATANO WA FAMILIA MOJA, YAJERUHI WENGINE WATANO


Watu watano wa familia moja wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi katika Kijiji cha Isangawane, Kata ya Matwiga, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya.


Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Jumapili, Desemba 29, 2024, wakati mvua kubwa iliyoambatana na radi iliponyesha kwa takriban saa mbili. Familia hiyo ilikuwa imelala kwenye zizi la kambi ya kuchungia ng’ombe.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga, amethibitisha vifo hivyo na kuwataja waliopoteza maisha kuwa ni Balaa Scania (28), Masele Masiganya (16), Hemi Tati (10), Manangu Ngwisa (18), na Kulwa Lawaje (10).


Majeruhi ni Manyenge Masagala (13), Serusi Solo (13), Paskalia Kalez (16), Gulu Scania (30), na Huruma Kalezi (19), wote wakiwa wakazi wa Kitongoji cha Nkinga, Kijiji cha Isangawane.


Diwani wa Kata ya Matwiga, Frank Mkondo, amesema eneo hilo limepimwa rasmi na serikali ya kijiji kwa ajili ya makazi. Hata hivyo, ukosefu wa zahanati umefanya majeruhi kutibiwa kwenye duka la dawa muhimu kabla ya kuruhusiwa kurudi nyumbani.


Tukio hili linaongeza idadi ya matukio ya vifo vinavyosababishwa na radi katika eneo hilo, ambapo mwezi huu pekee, mtu mwingine pia alipoteza maisha kutokana na radi.

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA