RAIS DKT. MWINYI AANIKA MAFANIKIO YA SMZ 2024
Katika hotuba yake ya kuuaga mwaka 2024 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2025, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Disemba 30,2024 ameeleza mafanikio makubwa yaliyopatikana katika sekta mbalimbali nchini. Alisisitiza umuhimu wa wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii ili kuharakisha maendeleo ya taifa.
Mafanikio katika Sekta za Uchumi na Miundombinu
Rais Dkt. Mwinyi alieleza mafanikio katika kukuza uchumi mijini na vijijini, kudhibiti ukusanyaji wa mapato, kuimarisha uwekezaji na biashara, ujenzi wa miundombinu ya barabara, viwanja vya ndege, bandari, nyumba za makazi, usambazaji wa huduma za umeme na maji safi, pamoja na uimarishaji wa sekta ya elimu na afya kote nchini.
Uwekezaji katika Sekta ya Utalii
Rais Dkt. Mwinyi pia alieleza mafanikio katika sekta ya utalii, akisema kuwa mafanikio haya yanaitangaza Zanzibar kimataifa.
Uboreshaji wa Sekta ya Elimu
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi alieleza ongezeko la bajeti ya mikopo ya elimu ya juu kutoka TZS bilioni 50 hadi TZS bilioni 100, ili kuwasaidia wanafunzi wengi zaidi kupata elimu ya juu.
Kwa kumaliza mwaka 2024, Rais Dkt. Mwinyi alisisitiza dhamira ya Serikali ya kuendelea kudumisha amani, umoja, na mshikamano wa kitaifa, na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika sherehe za kuadhimisha Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964.

Comments