SHERIA YA KIVITA KOREA KUSINI: MAANDAMANO NA VURUGU ZA KISIASA YAZIDI


 Helikopta ziliruka na vifaru kuonekana mitaani Seoul baada ya Rais Yoon Suk Yeol kutangaza sheria ya kijeshi katika hotuba ya ghafla usiku wa manane. 


Uamuzi huo umeibua maandamano makali tarehe 3 Dec 2024 kutoka kwa wapinzani wa kisiasa wanaoshutumu serikali yake kwa kuzorotesha demokrasia na kudhibiti bunge.


Waandamanaji walikusanyika karibu na bunge, huku polisi wakijaribu kuwazuia kuingia. Wanajeshi walilinda majengo ya Bunge.


Yoon aliahidi kulinda demokrasia ya kikatiba na kupambana na vitisho vya Korea Kaskazini, lakini hatua zake zimeongeza mgawanyiko wa kisiasa na ukosoaji wa upinzani.


Bunge limebatilisha tangazo hilo, lakini tamko la mwisho linategemea uamuzi wa baraza la mawaziri, hatua inayoweza kusababisha mkwamo mkubwa wa kisiasa.

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA