WAZIRI MKUU: TAMASHA LA BUHAYA NI NJIA YA KUKUZA UCHUMI NA UTAMADUNI
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa, amepongeza mchango wa Tamasha la Buhaya Festival katika kukuza utamaduni, mshikamano, na maendeleo ya kiuchumi kwa Mkoa wa Kagera.
Akihutubia tamasha hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, Waziri Mkuu alimsifu mchekeshaji maarufu Mama Mawigi kwa juhudi zake za kutangaza utamaduni wa Kagera. Alisema:
“Mama Mawigi amekuwa mfano wa kuigwa katika juhudi za kuitangaza Kagera. Sanaa na utamaduni vina nafasi kubwa siyo tu kwa burudani, bali pia kwa kuimarisha utalii na uchumi wa mkoa.”
Waziri Mkuu pia alizungumzia:
1. MAENDELEO YA KIUCHUMI:
Alieleza kuwa Kagera ina fursa kubwa kupitia kilimo, biashara, na utalii, akisisitiza umuhimu wa kutumia matukio kama Tamasha la Buhaya kuvutia wawekezaji.
2. UMOJA NA MSHIKAMANO:
Aliwataka watu wa Kagera kuendelea kushirikiana kwa ajili ya maendeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla.
3. VIPAJI NA AJIRA KUPITIA SANAA:
Alihimiza vijana kutumia sanaa kama fursa ya ajira huku wakihifadhi urithi wa kiutamaduni wa mkoa wao.
Tamasha la Buhaya limeendelea kuwa jukwaa muhimu kwa kuunganisha watu wa Kagera na kutangaza urithi wao wa kipekee ndani na nje ya Tanzania.

Comments