WESTFALENSTADION YA DORTMUND ITAKUWA MWENYEJI WA MKONDO WA PILI WA ROBO FAINALI YA LIGI YA MATAIFA YA UJERUMANI DHIDI YA ITALIA
Westfalenstadion ya Dortmund itakuwa mwenyeji wa mkondo wa pili wa robo fainali ya Ligi ya Mataifa ya Ujerumani dhidi ya Italia mnamo Machi 2025.
FA ya Ujerumani (DFB) imetangaza Disemba 12, 2024 kuwa Mechi hiyo itafanyika katika uwanja wa nyumbani wenye viti 82,000 wa Borussia Dortmund mnamo Machi 23, siku tatu baada ya mechi ya mkondo wa kwanza huko San Siro ya Milan. Katika taarifa yake, mkurugenzi wa michezo wa DFB, Rudi Voeller alisema: "Dortmund ni eneo linalofaa kwa mchezo wa soka."
Ujerumani, ambao wamo katika mtoano wa Ligi ya Mataifa kwa mara ya kwanza, walishinda mchezo wao wa hivi majuzi zaidi kwenye uwanja huo, ushindi wa 2-0 dhidi ya Denmark katika hatua ya 16 bora ya Euro 2024.

Comments