BASHE AONGOZA TANZANIA KUPITISHA PROGRAMU YA KILIMO AFRIKA (CAADP 2026-2035)
Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb.), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Umoja wa Afrika uliofanyika Uganda kuanzia tarehe 9 hadi 11 Januari 2025. Mkutano huo ulilenga kupitisha Programu ya Kuendeleza Kilimo Barani Afrika (CAADP) kwa kipindi cha 2026 hadi 2035.
Katika ujumbe wake, Mhe. Bashe aliongozana na Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa H. Aweso (Mb.), Waziri wa Kilimo wa Zanzibar, Mhe. Shamata Shaame Khamis, na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Alexander P. Mnyeti.
Mhe. Bashe alisisitiza umuhimu wa uwekezaji wa pamoja katika sekta ya kilimo kwa lengo la kufikia uhuru wa chakula, kuboresha mifumo ya uzalishaji, na kulinda mazingira. Programu ya CAADP imekuwa msingi wa maendeleo ya kilimo Afrika tangu 2003, ikilenga kuongeza usalama wa chakula na kupunguza umaskini vijijini.


Comments