BURKINA FASO YATENGENEZA GARI LAKE LA KWANZA KWA 100% BILA MSAADA WA NJE
Gari linatumia umeme, chaji ya dakika 30 inasafiri hadi kilomita 330
Burkina Faso, chini ya uongozi wa Captain Ibrahim Traoré, imeandika historia kwa kutengeneza gari lake la kwanza kwa asilimia 100 bila msaada kutoka nje. Wahandisi wa nchi hiyo wamefanikiwa kubuni na kutengeneza gari la umeme ambalo likichajiwa kwa dakika 30 pekee, linaweza kusafiri umbali wa kilomita 330 – sawa na safari kutoka Dar es Salaam hadi Tanga.
Hatua hii ni mafanikio makubwa kwa Burkina Faso, taifa ambalo limekuwa likijitahidi kujitegemea kiteknolojia na kiuchumi. Gari hilo la umeme linathibitisha maendeleo ya sekta ya viwanda barani Afrika, huku likiwa mfano wa uvumbuzi unaoweza kusaidia kupunguza utegemezi wa mafuta na kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Serikali ya Burkina Faso inatarajiwa kutumia teknolojia hii kuimarisha sekta ya usafiri na uchumi wa ndani, huku ikiendelea kuhamasisha maendeleo ya viwanda vya ndani kwa lengo la kuifanya nchi hiyo kuwa kitovu cha teknolojia ya magari ya umeme barani Afrika.

Comments