CHINA YAJENGA KITUO KIKUBWA CHA NISHATI YA NYUKLIA KULIKO CHA MAREKANI
China inajenga kituo kikubwa cha muunganiko wa nyuklia (nuclear fusion) ambacho kinakadiriwa kuwa na ukubwa wa asilimia 50 zaidi ya Kituo cha Kitaifa cha Mwako cha Marekani (National Ignition Facility - NIF).
Kituo hiki kipya kinalenga kuendeleza teknolojia ya nishati safi ya nyuklia kupitia muunganiko wa atomu, mbinu inayojaribu kuiga mchakato wa nishati ya jua. Ikiwa utafiti huu utafanikiwa, unaweza kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya nishati kwa kutoa chanzo cha nishati kisicho na uchafuzi wa mazingira na chenye ufanisi mkubwa.
Hatua hii inaifanya China kuendelea kuongoza katika mbio za kisayansi na kiteknolojia za nyuklia, huku ikizidi kushindana na Marekani na mataifa mengine katika utafiti wa nishati endelevu ya siku zijazo.

Comments