DONALD TRUMP AAPISHWA RASMI KUWA RAIS WA 47 WA MAREKANI


 

Donald Trump ameapishwa rasmi kuwa Rais wa 47 wa Marekani leo, Januari 20, 2025, akitimiza moja ya comebacks kubwa kisiasa katika historia. Katika umri wa miaka 78, Trump anakuwa rais mzee zaidi kuongoza taifa hilo.


Hafla ya kuapishwa ilifanyika ndani ya Rotunda ya Jengo la Capitol kutokana na hali ya hewa ya baridi kali. Kiapo cha uongozi kilitolewa na Jaji Mkuu John Roberts. Tukio hilo liliudhuriwa na viongozi wa kisiasa, watu mashuhuri, pamoja na mabilionea wa teknolojia kama Elon Musk, Jeff Bezos, na Mark Zuckerberg.


Katika hotuba yake ya kwanza, Trump alitangaza kuanza kwa “enzi ya dhahabu ya Marekani” huku akiahidi kulipa kipaumbele taifa lake. Alisema, chini ya uongozi wake, Marekani haitanyanyaswa na mataifa mengine.


Mara baada ya kuapishwa, Rais Trump anatarajiwa kusaini maagizo kadhaa ya rais yanayolenga masuala kama usalama wa mipaka, maendeleo ya mafuta na gesi, na kufuta mipango ya usawa wa kijamii. Pia ameahidi kutangaza hali ya dharura kitaifa katika mpaka wa kusini na kufuta sera nyingi za utawala uliopita.


Tukio hilo liliangukia siku ya kumbukumbu ya Martin Luther King Jr. Wakati wa hafla hiyo, mtangazaji wa CBS, Gayle King, alibainisha ukosefu wa watu wenye asili ya Kiafrika miongoni mwa waliohudhuria, akisema hili ni jambo muhimu katika historia ya Marekani. Trump alitambua siku hiyo katika hotuba yake na kuahidi kufanya kazi kufanikisha ndoto za King.


Usalama ulikuwa umeimarishwa sana katika mji wa Washington, D.C., kwa kuwepo polisi na wanajeshi kuhakikisha amani na usalama wa hafla hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA