DONALD TRUMP KUAPISHWA LEO KUWA RAIS WA 47 WA MAREKANI


Donald Trump ataapishwa leo, Januari 20, 2025, kuwa Rais wa 47 wa Marekani katika hafla itakayofanyika katika Rotunda ya Jengo la Capitol, Washington, D.C. Sherehe hiyo itaanza saa 12:00 jioni (EST), sawa na saa 8:00 usiku kwa Afrika Mashariki.


Jaji Mkuu John Roberts atamuapisha Trump, huku Jaji Brett Kavanaugh akimuapisha Makamu wa Rais mteule, JD Vance. Baada ya kuapishwa, kutakuwa na hotuba, chakula cha mchana rasmi, na gwaride kuelekea Ikulu ya White House.


Matangazo ya moja kwa moja yataonyeshwa kupitia vituo mbalimbali, ikiwemo VOA Swahili.

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA