MJI WA GOMA DRC WATEKWA NA M23


Kufuatia machafuko yanayoendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), uongozi wa Alliance Fleuve Congo (AFC) unatoa taarifa kwa umma kuhusu hatua zifuatazo:

1. Kukamatwa kwa Jiji la Goma:

Vikundi vya waasi vya M23, vinavyodaiwa kuungwa mkono na Rwanda, vimekamatwa jiji kuu la Goma, mji mkubwa mashariki mwa DRC. Hali hii imeongeza wasiwasi kuhusu usalama katika eneo hilo na kuathiri zaidi wakazi wa Goma. 

2. Mwito kwa Utulivu:

Tunatoa wito kwa wakazi wote wa Goma na maeneo mengine yaliyoathiriwa na machafuko kuwa watulivu. Ukombozi wa jiji hili umefanyika kwa mafanikio, na hali ya usalama iko chini ya udhibiti.

3. Kusimamishwa kwa Shughuli za Ziwa:

Kuanzia sasa, shughuli zote za ziwa zinasitishwa hadi ilani nyingine, ili kudumisha utulivu na usalama katika mji wa Goma na maeneo ya jirani.


"Tunasisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika kutatua mgogoro huu na kurejesha amani katika eneo la Maziwa Makuu."

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA