MKATABA UNAOMTESA CONGO DRC DHIDI YA RWANDA: KONGO DRC KUWEKWA MIKONONI MWA RWANDA, UGANDA, ETHIOPIA NA SUDANI KUSINI


Huu ni mkataba ambao umeendelea kumtesa Congo DRC na kuonesha wazi jinsi ulivyoshindwa kuleta umoja na utulivu katika nchi hiyo. Mapema usiku wa tarehe 16/3/1996, viongozi kutoka Rwanda, Uganda, Sudan Kusini, na Ethiopia pamoja na kiongozi wa AFDL, Laurent Kabila, walitia saini “Makubaliano ya Mkataba wa Lemera”.


Mkataba huu ulilenga kuigawa nchi ya Congo mikononi mwa Marekani kwa kupitia usimamizi wa mataifa hayo ya Rwanda, Uganda, Sudan Kusini na Ethiopia, huku Kenya na Tanzania zikiwa na nafasi muhimu katika kuanzisha mkataba huo. Ingawa baadaye Tanzania ilijitoa kuunga mkono mpango huo wa kugawa Kongo, iliamua kusimama upande wa Laurent Kabila, ambaye alikataa kutekeleza mkataba wa Lemera.


Kwa mujibu wa mkataba huo, operesheni maalum ya kijeshi ilianzishwa inayoitwa “Operation Banyamrenge” ambayo ilikuwa na lengo la kumuondoa madarakani Mobutu Sese Seko, ambaye alikuwa kiongozi wa muda mrefu wa Kongo na kibaraka wa Marekani. Wakati huo, Mobutu alichoshwa na mabadiliko ya kisiasa duniani, jambo lililochangia kuanzishwa kwa mapigano.


Katika makubaliano yaliyofikiwa kati ya Laurent Kabila na mataifa hayo, Kabila ambaye aliongoza chama cha “kuikomboa Kongo” alikubaliana na masharti kadhaa, yakiwemo ya kushirikiana na wapiganaji wa Kinyarwanda kutoka Rwanda, Uganda, na Watusi waliokuwa na makazi mashariki mwa Kongo. Baada ya mapigano, Kabila alikubali kutoa sehemu ya ardhi ya mashariki mwa Kongo kama shukrani kwa Rwanda na Uganda. Aliruhusu pia usalama wa taifa la Kongo kuwa chini ya udhibiti wa mataifa haya.


Makubaliano hayo yalifanyika katika vilima vya Lemera, vilivyoko Kivu ya Kusini, katika mji wa Uvira, na yakawekwa kwenye historia kama “Mkataba wa Lemera”. Mkataba huu ulitaka Kabila, baada ya kuwa rais wa Kongo, kuruhusu mikoa miwili ya Kivu Kaskazini na Kusini kuwa makazi ya Wanyarwanda wa kabila la Kitutsi. Hii ililenga kumweka Kongo chini ya udhibiti wa Rwanda na Uganda, kwa kutoa maeneo muhimu ya kijiografia kwa faida zao za kiusalama na kiuchumi.

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA