RAIS DKT. SAMIA AIPONGEZA TIMU YA YANGA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameipongeza Klabu ya Yanga kwa ushindi wake kwenye mchezo wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika (CAF Champions League).
Kupitia salamu zake, Rais Samia amesema:
“Pongezi kwa Klabu ya Yanga kwa ushindi katika mchezo wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika. Mnaendelea kuleta furaha kwa Watanzania huku mkilitangaza vyema jina la nchi yetu kimataifa. Ninawatakia kila la kheri.”
Huu ni mwendelezo wa kutambua juhudi za wanamichezo nchini na mchango wao katika kuipa sifa Tanzania kwenye anga za kimataifa.

Comments