RAIS MWINYI KUTUNUKU ZANZIBAR HEROES KWA CHAKULA CHA MCHANA IKULU
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi, ameialika Timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, kwa chakula cha mchana Ikulu siku ya Jumatano, tarehe 15 Januari 2025.
Mwaliko huo umetolewa na Rais Mwinyi kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba, baada ya Zanzibar Heroes kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Michuano ya Mapinduzi 2025 kwa kuifunga Burkina Faso magoli 2-1 katika mchezo wa fainali uliovutia mashabiki wengi.
Rais Mwinyi, aliyekuwa mgeni rasmi wa fainali hiyo, alikabidhi kombe kwa mabingwa hao huku akisifu juhudi zao kubwa za kuipeperusha vyema bendera ya Zanzibar.
SAFARI YA UBINGWA
Zanzibar Heroes ilitinga fainali baada ya kuilaza Timu ya Taifa ya Kenya, Harambee Stars, kwa goli 1-0 katika nusu fainali.
Mbali na kombe, timu hiyo pia imejishindia zawadi ya shilingi milioni 100 kama sehemu ya mafanikio yao katika michuano hiyo ya kihistoria.
Mwaliko wa Ikulu ni ishara ya shukrani na kuthamini mchango wa vijana wa Zanzibar katika kuiletea nchi heshima kimichezo.


Comments