RAIS MWINYI: MAPINDUZI YA ZANZIBAR YAMELETA MAFANIKIO MAKUBWA
Akizungumza leo Januari 12, 2025 ikiwa ni siku ya maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika kwenye uwanja wa Gombani, Pemba, Dkt. Mwinyi alitaja mafanikio hayo kuwa ni pamoja na:
1. Mageuzi ya kiuchumi – Kuimarisha upatikanaji wa mapato na kudhibiti matumizi yake.
2. Miundombinu – Kuimarisha barabara, viwanja vya ndege, sekta ya michezo, afya, umeme, na maji.
3. Ustawi wa kijamii – Kuimarisha biashara, huduma za afya, na kuhakikisha utawala bora na demokrasia.
Aidha, Rais Mwinyi aliwasihi Wanazanzibari kutumia maadhimisho haya kama kumbukumbu ya ushindi wa kujikomboa kiuchumi, kisiasa, na kijamii. Pia aliwataka kuendelea kuwakumbuka waasisi wa Mapinduzi, akiwemo Hayati Abeid Amani Karume na viongozi wenzake.
Kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka huu, Rais Mwinyi amewataka Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla kushiriki kwa amani na utulivu huku akisisitiza vyombo vya mamlaka kusimamia uchaguzi kwa haki na usawa.

Comments