TANZANIA KUPOKEA WAKUU WA NCHI 53 WA AFRIKA KATIKA MKUTANO M300
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Dkt. Khatibu Kazungu, amesema Tanzania imejipanga kikamilifu kupokea ugeni wa Wakuu wa Nchi 53 wa Afrika katika Mkutano wa Kimataifa wa M300.
Mkutano unatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania, kuanzia tarehe 27 hadi 28 Januari 2025.  Katika mkutano huo, Wakuu wa Nchi 53 wa Afrika watajadili mikakati ya kuharakisha upatikanaji wa nishati barani Afrika, hususan kwa Waafrika wapatao milioni 685 ambao bado hawana nishati ya umeme ikiwa ni sehemu ya juhudi za bara la Afrika kuelekea matumizi endelevu ya vyanzo vya umeme vinavyohifadhi mazingira.
Mkutano huu ni fursa kubwa kwa Tanzania kuonyesha mafanikio yake katika sekta ya nishati na kushirikiana na mataifa mengine kuboresha upatikanaji wa nishati barani Afrika. Aidha, ugeni huu utatoa nafasi ya kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na ushirikiano wa kiuchumi kati ya mataifa ya Afrika.


Comments