TRUMP AIONYA BRICS: USHURU WA 100% KWA HATUA ZA KUONDOA DOLA



Rais wa Marekani Donald Trump ameonya tena mataifa ya BRICS, akisema watakabiliwa na ushuru wa 100% katika biashara na Marekani iwapo wataendelea na juhudi za kupunguza matumizi ya dola katika biashara ya kimataifa.


Akizungumza kutoka Ikulu ya Marekani, Trump alisema:

“Kama taifa la BRICS, watachukua hatua hiyo basi tutawatoza ushuru wa 100% na wataachana nayo mara moja.”


Trump alisisitiza kuwa kauli yake si tishio bali msimamo thabiti wa Marekani katika kulinda nguvu ya dola kwenye biashara ya dunia.


BRICS, inayojumuisha mataifa kama Brazil, Urusi, India, China, Afrika Kusini, pamoja na wanachama wapya kama Misri na Iran, imekuwa ikijadili mbinu za kutumia sarafu za ndani kwa biashara kati ya wanachama wake.


Trump pia alijibu kauli za Rais wa zamani Joe Biden, ambaye alidokeza kuwa Marekani ipo katika hali ya hatari kuhusu suala hili, akisema:

“Biden anasema wao wana nguvu juu yetu, lakini ukweli ni kwamba sisi tuna nguvu juu yao, na hawataweza kufanikisha mipango yao.”


Msimamo huu unaashiria ongezeko la mvutano kati ya Marekani na BRICS kuhusu ushawishi wa kiuchumi duniani.

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA