TSHISEKEDI ATISHIA KUITANGAZIA RWANDA VITA KWA SABABU YA M23
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Félix Tshisekedi, amesema kuwa suluhisho la amani nchini mwake ni kuingia vitani dhidi ya Rais wa Rwanda, Paul Kagame, akimtuhumu kwa kuhusika na uasi wa kundi la M23 linalosababisha machafuko mashariki mwa DRC.
Katika hotuba yake, Tshisekedi alisisitiza kuwa endapo kutatokea mashambulizi mengine, ataitisha bunge la DRC na kuomba idhini rasmi ya kutangaza vita dhidi ya Rwanda.
“Suluhisho la amani DRC ni kuanzisha vita dhidi ya Paul Kagame. Nimesema, endapo kutatokea mashambulizi mengine, nitaitisha mabaraza mawili ya bunge kwa mujibu wa katiba na nitawaomba idhini ya kutangaza vita dhidi ya Rwanda,” alisema Tshisekedi.
Kauli hii inakuja wakati mgogoro kati ya DRC na Rwanda ukizidi kupamba moto, huku M23 ikiendelea kushikilia maeneo kadhaa mashariki mwa Kongo, jambo linalosababisha maelfu ya watu kukimbia makazi yao. Rwanda kwa upande wake imekana mara kadhaa kuhusika na kundi hilo, lakini uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeendelea kuwa mbaya.

Comments