UBALOZI WA UGANDA MJINI KINSHASA WAPORWA NA KUCHOMWA MOTO NA WAANDAMANAJI


 Waandamanaji nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wamevamia na kuchoma moto Ubalozi wa Uganda uliopo mjini Kinshasa, wakionesha ghadhabu yao dhidi ya kile wanachodai ni ushirikiano wa mataifa jirani katika mgogoro wa waasi wa M23.


Tukio hilo limekuja wakati hasira za wananchi wa DRC zikizidi kuongezeka kutokana na mashambulizi ya M23, kundi ambalo serikali ya Kongo inadai linaungwa mkono na mataifa jirani, hususan Rwanda.


Pamoja na Ubalozi wa Uganda kuporwa na kuchomwa moto, maandamano hayo pia yalishuhudia waandamanaji wakipambana na vikosi vya usalama katika maeneo mbalimbali ya Kinshasa.


Serikali ya Uganda bado haijatoa tamko rasmi kuhusu tukio hilo, lakini hali ya uhusiano kati ya DRC na nchi jirani inazidi kuwa tete, huku taharuki ikitanda katika ukanda wa Maziwa Makuu.

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA