NORD-UBANGI: ZAIDI YA WATU 7,000 WA AFRIKA YA KATI WAKIMBIA KISASI CHA WAASI CAR, WAKIWA KATIKA HALI NGUMU BOSOBOLO
Tangu Desemba 2024, maelfu ya raia wa Afrika ya Kati wamekuwa wakivuka Mto Ubangi wakikimbia ukatili wa waasi wa Seleka nchini CAR, wakitafuta hifadhi katika eneo la Gbando, Bosobolo, DRC.
Wakimbizi hawa, wakiwemo wanawake wajawazito na watoto chini ya miaka mitano, wanakabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu. Wanalala nje bila makazi, huku maji pekee wanayotumia ni kutoka Mto Ubangi, jambo linalozua hofu ya magonjwa na usalama wao.
Mamlaka ya eneo hilo imethibitisha kuwa zaidi ya watu 7,000 tayari wamekusanyika Gbando, lakini hawajapewa msaada wowote. Tume ya Kitaifa ya Wakimbizi (CNR) imeanzisha tathmini ili kubaini ikiwa watapewa hadhi rasmi ya ukimbizi.
Hali hii imesababishwa na mauaji ya kiongozi wa waasi wa Seleka na jeshi la CAR, ambapo waasi wameapa kulipiza kisasi, hivyo kuwalazimisha raia wa kawaida kukimbia makazi yao.

Comments