US / MAREKANI YAONGOZA MAJADILIANO YA USALAMA YA KIKANDA BAHRAIN


Amri Kuu ya Marekani (CENTCOM) imeongoza mazungumzo ya usalama wa kikanda yaliyoandaliwa na Jeshi la Ulinzi la Bahrain, yakiwakutanisha viongozi wa kijeshi na ulinzi kutoka mataifa 12 ya Mashariki ya Kati.


Kamanda wa CENTCOM, Brad Cooper, pamoja na maafisa waandamizi wa kijeshi kutoka Bahrain, Egypt, Jordan, Kuwait, Lebanon, Oman, Qatar, Saudi Arabia, Syria, United Arab Emirates na Yemen, walijadili hali ya usalama wa kikanda na njia za kuimarisha ushirikiano wa ulinzi.


Viongozi hao walisisitiza umuhimu wa kulinda uhuru wa usafiri na biashara kupitia Strait of Hormuz, njia muhimu ya kimataifa ya usafirishaji wa mafuta na bidhaa nyingine.


Kwa mujibu wa CENTCOM, Marekani na washirika wake wanaendesha mfumo mkubwa wa pamoja wa ulinzi wa anga na makombora katika Mashariki ya Kati. Pia, mwezi Januari, walizindua kitengo kipya cha uratibu wa ulinzi wa anga kwa ajili ya kubadilishana taarifa za vitisho na kuratibu hatua za dharura.


Mkutano huo umeweka historia kwa kuwa mara ya kwanza viongozi wa kijeshi kutoka Syria na Lebanon kushiriki katika mazungumzo ya ulinzi wa kikanda yanayoongozwa na Marekani.


#USSecurity #MiddleEast #CENTCOM #Bahrain #RegionalDefense

Comments

Popular posts from this blog

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO