Posts

VIDEO PRODUCTION, GRAPHICS &DESIGN

Image
 Watayarishaji wa video za matukio yote Rasmi, sherehe za Harusi, Sherehe za Send Off, Komunio, Kipaimara, Siku ya Kuzaliwa, Maadhimisho ya kumbukizi,  filamu, tamthiliya n.k  Usanifu wa:  Nembo, Bango, vipeperushi, Matangazo,kalenda, jarida na vitabu n.k.📞+255 714 850 988  🌐nicaproductsandservices@gmail.com

WAZIRI MKUU MGENI RASMI BUHAYA FESTIVAL

Image
 WATANZANIA TULINDE UTAMADUNI WETU KWA FAIDA YA VIZAZI VIJAVYO   WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wahakikishe wanalinda utamaduni na kujenga misingi ya kuhamasisha vijana na vizazi vijavyo kutambua na kuenzi historia na urithi wa Mtanzania. Amesema kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kutunza utamaduni, mila na desturi kwa sababu utamaduni ni nguzo ya utambulisho wa jamii husika na ni muhimu kwa kizazi kijacho. Amesema hayo leo (Jumapili, Oktoba 27, 2024) wakati akifungua Tamasha la Buhaya 2024 ‘Buhaya Festival’ lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam. “Katika siku za sasa, ambapo teknolojia na utandawazi vinazidi kuimarika, ni rahisi kupoteza mila na desturi zetu, hivyo tunaposhiriki tamasha hili, tunajifunza na kuhamasisha jamii zetu kuhusu umuhimu wa urithi wetu wa kiutamaduni.” Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amewaasa wazazi, jamii na madhehebu ya dini kuendelea kuhimiza utunzaji wa maadili kwa kuzingatia mila na desturi ili kuepuka mmo...

MILANGO YA RAIS SAMIA IKO WAZI, ANAWAKARIBISHA VIONGOZI WA DINI: DKT. BITEKO

Image
📌 *Dkt. Biteko Amwakilisha Rais Samia Jubilei ya Miaka 50 ya AICT Magomeni* 📌*Rais Samia Achangia Milioni 100 Ujenzi wa Kanisa* 📌*Awahimiza Waaumini Kujitoa Kujenga Kanisa* 📌 *Atoa Wito kwa Viongozi wa Dini Kutimiza Kusudi la Mungu* 📌 *Awahimiza Watanzania Kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, Mwaka huu* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan yuko tayari  kuendelea kushirikiana na  viongozi wa dini kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali kuhusu maendeleo na ustawi wa nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Oktoba 27, 2024 Jijini Dar es salaam wakati akimwakilisha Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ibada maalum ya shukrani ya kuadhimisha miaka 50 ya Pastoreti ya AICT Magomeni. “ Mhe. Rais anakumbuka namna mnavyomshirikisha  katika masuala mbalimbali yanayohusu kanisa na kwa kweli milango yake iko wazi anawakaribisha  wakati wowote ili muw...

TANZANIA KUBADILI NOTI ZA FEDHA NA ALAMA ZAKE

Image
Benki Kuu ya Tanzania imeeleza kuwa serikali imeamua kuondoa kwenye mzunguko baadhi ya noti za zamani za shilingi ya Tanzania zilizotolewa kati ya mwaka 1985 hadi 2003 na noti ya shilingi mia tano iliyotolewa mwaka 2010.  Tangu ilipoanzishwa mwaka 1966, Benki Kuu ya Tanzania imetoa matoleo mbalimbali ya noti na sarafu.Kwa historia ya matoleo ya Noti na sarfu zilizotolewa na Benki kuu ya Tanzania. Noti hizi ni zile zenye alama maalum ya kutambua thamani ya shilingi ishirini, mia mbili, mia tano, elfu moja, elfu mbili, elfu tano, na elfu kumi. Kuanzia tarehe 6 Januari 2025 hadi 5 Aprili 2025, wananchi wataweza kuweka au kubadilisha noti hizo kupitia benki na taasisi za kifedha, lakini mchakato huu utafanyika tu katika ofisi kuu na matawi ya benki na taasisi za kifedha, na hautafanyika kupitia mawakala. Benki Kuu imetangaza kuwa itawapa mafunzo wafanyakazi wa benki na taasisi za kifedha ili kuhakikisha noti feki hazihusishwi katika zoezi hili.  Wataelekezwa kuzingatia miongozo ya...

VIKOSI VYA ISRAEL VINAWASHIKILIA MADAKTARI NA WAGONJWA BAADA YA UVAMIZI KATIKA HOSPITALI YA GAZA

Image
 VIKOSI VYA ISRAEL VINAWASHIKILIA MADAKTARI NA WAGONJWA BAADA YA UVAMIZI KATIKA HOSPITALI YA GAZA Vikosi vya Israel vimeondoka katika Hospitali ya Kamal Adwan baada ya kuwazuilia makumi ya madaktari na baadhi ya wagonjwa, na kusababisha uharibifu mkubwa katika moja ya hospitali zinazofanya kazi kaskazini mwa Gaza. Wizara ya Afya katika eneo lililozingirwa imesema Kituo hicho cha matibabu kiko katika hali mbaya baada ya kuvamiwa na kushambuliwa kwa makombora katikati ya mashambulio ya wiki tatu ya Israel kaskazini, huku afisa wa ngazi ya juu wa Wizara ya Afya ya Gaza akitoa wito kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) kuwahamisha majeruhi kutoka hospitali hiyo inayochukuliwa kuwa njia ya kuokoa maisha ya watu wanaoishi katika eneo hilo.  kaskazini mwa Gaza.  "Harufu ya kifo imeenea karibu na hospitali," Marwan al-Hams, mkurugenzi wa hospitali za shamba katika Wizara ya Afya ya Gaza, amesema vikosi vya Israeli viliharibu vifaa vya matibabu vya hospitali wakati wa uvamizi wao ili ...

MAGAZETI YA LEO NCHINI TANZANIA

Image
Karibu kusoma kurasa za mbele za magazeti ya leo tarehe 27/10/2024  

WAZIRI MKUU AIKABIDHI TAKUKURU MAGARI 88

Image
WAZIRI MKUU AIKABIDHI TAKUKURU MAGARI 88 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 26, 2024 amekabidhi magari mapya 10 ikiwa ni ishara ya kukabidhi magari 88 yaliyonunuliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) ambayo yatasambazwa mikoani kwa lengo la kuongeza tija na kuboresha utendaji kazi wa Taasisi hiyo. Akitoa taarifa ya magari hayo, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Chalamila amemweleza Waziri Mkuu kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan madarakani, TAKUKURU imepatiwa jumla ya Shilingi bilioni 30 za kununulia magari 195 ambapo 88 yameshanunuliwa. “Mchakatio wa kununua magari 107 yaliyobakia unaendelea na tunatarajia kuyapata hivi karibuni, tunaahidi kutatunza magari haya ili kuongeza tija katika utendaji wetu” Amesema  Bw. Crispin Waziri Mkuu amekabidhi magari hayo wakati anafunga mafunzo ya awali ya uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU), hafla hiyo inafanyika kwenye Shule ya Po...

KURASA ZA MBELE ZA MAGAZETI YA LEO

Image
  Karibu kusoma kurasa za mbele za magazeti ya leo tarehe 26/10/2024

HAMAS YATOA WITO KUKOMESHA MAUAJI YA KIMBARI

Image
    HAMASI YATOA WITO KUKOMESHA  MAUAJI  YA KIMBARI   Kundi la wapiganaji wa Palestina (Hamas) linatoa        wito kwa viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu kuchukua hatua kukomesha mauaji ya kimbari dhidi ya watu wao.  Hamas imesema hayo jana tarehe 25 Oktoba 2024  baada ya jeshi la uvamizi la kigaidi kuvamia hospitali ya Shahidi Kamal Adwan iliyopo katika mradi wa Beit Lahia, saa chache baada ya kuizingira na kuwakamata na kuwatesa wagonjwa, na majeruhi wakiwemo wahudumu wa afya pamoja na kuhamisha familia za wanaharakati wa vyombo vya habari, na kuwapeleka kusikojulikana jambo ambalo ni uhalifu wa kivita na   ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa. Aidha, Hamas imewataka viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu kubeba majukumu yao, kutoridhika na kauli za kulaani na badala yake kuanza kuchukua hatua za kukomesha vita vya mauaji ya kimbari na mauaji ya kikabila ambayo watu wao wanafanyiwa.  Hamas imeeleza kuwa serikali...

VIONGOZI WA JUMUIA YA MADOLA WAKUTANA PACIFIC

Image
VIONGOZI WA JUMUIA YA MADOLA  WAKUTANA PACIFIC Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola (Common Wealth) wa 2024 umefunguliwa rasmi leo Ijumaa, Oktoba 25, katika visiwa vya Pacific huko Samoa. Aidha, Viongozi wa Jumuiya hiyo watakutana  tena juma lijalo kuendelea na Mkutano huo. Kwa kipindi hiki ni zamu ya Afrika kupata nafasi ya Katibu Mkuu baada ya miaka 20 kupita, huku kukiwa na utata kuhusu iwapo malipo ya fidia yanapaswa kujumuishwa kwenye ajenda za mkutano huo au la. Wagombea watatu wanawania nafasi hiyo ya juu ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Ghana Shirley Ayorkor Botchwey; Waziri wa zamani wa biashara na viwanda wa Lesotho Joshua Phoho Setipa; na Waziri wa Mambo ya Nje wa Gambia Mamadou Tangara . Rwanda inatoa wito kwa chama hicho chenye wanachama 56 kufanya kazi kwa bidii zaidi ili kuondokana na "vikwazo na upendeleo" unaoendelea kuwarudisha nyuma wanawake na wasichana. Je nini kitajiri? endelea kufuatilia katika blog hii.