RAIS WA UKRAINE AMSHUKURU MWANAMKE ALIYEJITOKEZA KUPINGA VITA
Rais wa Ukraine Zelenskyy amemshukuru mwanamke wa Urusi baada ya kukimbilia kwenye seti ya taarifa ya moja kwa moja ya habari ya TV na bango la kupinga vita jana Jumatatu jioni. Siku ya Jumatatu jana jioni, wakati wa taarifa ya moja kwa moja ya habari kwenye Channel 1 inayomilikiwa na serikali ya Urusi, mhariri mwanamke aliyeshikilia bango la kupinga vita alikimbilia kwenye seti na kusimama nyuma ya manga. Bango hilo lilisomeka, “Hakuna vita, acha vita, propaganda hizo, wanakudanganya hapa” Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Marina Ovsyannikova, alikamatwa baadaye na kwa sasa yuko chini ya ulinzi wa polisi kama ilivyoripotiwa hapo awali. Hapo awali, alirekodi video ambayo aliitaja uvamizi wa Urusi kama "uhalifu" na akasema alikuwa na aibu kazi ya "propaganda za Kremlin" Rais wa Ukrain Volodymyr Zelenskyy alimshukuru na kusema anashukuru kwa Warusi wote "ambao hawaachi kujaribu kueleza ukweli" Katika taarifa yake ya video, Rais Zelenskyy alisema, ...