MGOGORO MASHARIKI MWA DRC: JUMUIYA YA KIMATAIFA YALAUMIWA, MICHATO YA AMANI YAKWAMA, NA SERIKALI YAKOSOLEWA
Wakati jumuiya ya kimataifa na mataifa ya kanda yakihimiza kurejelewa kwa mazungumzo kati ya Kinshasa na Kigali, hali bado haijatatuliwa, hasa baada ya kufutwa kwa mkutano wa pande tatu mjini Luanda. Ingawa Kinshasa inaonekana kushikamana na mchakato huo, Rais wa Rwanda, Paul Kagame, amejitenga nao, akizidisha ukosoaji wake dhidi ya upatanishi unaoongozwa na Angola. Baada ya waasi wa M23, wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda, kuteka mji wa Goma na kupanua udhibiti wao katika Kivu Kaskazini, Jason Stearns, mkurugenzi wa Kikundi cha Utafiti cha Kongo (CSG), alitoa tathmini ya mgogoro huo mnamo Januari 31 2025. JUMUIYA YA KIMATAIFA YANUFAISHA RWANDA Stearns anaamini kuwa jumuiya ya kimataifa imekuwa na mtazamo wa kuridhika kuelekea Rwanda, hali ambayo imesababisha kuzorota kwa mgogoro huo. “Tunapaswa kurudi nyuma kidogo katika historia ili kuelewa tumefikaje hapa. Katika mashambulizi ya M23 ya kwanza mwaka 2012-2013, wafadhili walipunguza msaada wa Rwanda kwa zaidi ya dola milioni 240 ndani...